Tuesday, October 25, 2011
Muuza nyama kutoka moja ya mabucha yaliyopo Soko Kuu la Manispaa ya Songea aliyefahamika kwa jina moja la Heddy akiuchapa usingizi baada ya kusubiri wateja kwa muda mrefu bila ya mafanikio,ulazi wa kitoweo hicho katika mji wa songea unazidi kupungua kufuatia ongezeko la bei kutoka ths 4000 hadi 5000 kwa kilo.
PAMBANO LA KIRAFIKI
Bondia Mussa Omari wa Songea kushoto,akimpiga ngumi bondia Mohamed Matumla kulia ambaye ni mtoto wa bondia mkongwe Rashid Matumla katika pambano lao lisilokuwa na ubingwa wowote lililofanyika katika uwanja wa majimaji siku Idd el Fitri mjini Songea juzi,ambapo mabondia hao walitoshana nguvu kwa kutoka sare,
ICE CREAM
,Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Majengo katika Manispaa ya Songea wakila askrim kwa ajili ya kupoza kiu.
Thursday, October 20, 2011
Wednesday, October 12, 2011
SIKUKUU YA MASHUJAA-SONGEA
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa,akitoa heshima katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa vita ya Majimaji wakati wa siku ya Mashujaa ambayo kwenye ngazi ya mkoa ilifanyika Mjini Songea.
BAADA YA MLO SHULE INAENDELEA
wanafunzi wa shule ya msingi kawawa manispaa ya Songea ambao hawakufahamika mara moja ni wa darasa la ngapi wakila kande wakati wa mapumziko yao ya saa nne katika kibanda kimojawapo cha mama lishe kilichopo jirani na shule hiyo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu mjini songea,
MWACHIENI YUPO HURU
,Hakimu mkazi mfawidhi wa mahama ya mkoa Ruvuma,Batisita Muhelela,akiwasihi polisi wasiendelee kumshikilia bw mohamedi nditi aliyekaa chini ambaye alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuvunja na kuiba ambapo aloifutiwa mashitaka baada ya kukosekana ushahidi,
CHINI YA ULINZI
Askari polisi wakimdhibiti Bw Mohamedi nditi katikati ili asikimbie baada ya jaribio lake la kutaka kutoroka chini ya ulinzi wa polisi hao kushindikana jana mbele ya mahakama ya mkoa Ruvuma,
TUKIO LA KIMILA-KILWA
Baadhi ya wajukuu kati ya wajukuu 100 wa marehemu Jumbe Mshamu mmanja,wakishika jiwe mojawapo la kaburi la babu yao aliyefariki miaka 150 iliyopita ambalo liko zaidi ya km 5 kutoka barabara kuu ya Kibiti Lindi eneo la kijiji cha Kiranjeranje wilayani Kilwa juzi ikiwa ni shara ya kumkumbuka na kumuombea kwa lengo la kupata baraka zake,
TUKIO LA KIMILA-KILWA
Mzee Abderehaman Amri,kulia akicheza ngoma ya kindimba linalochezwa na kabila la wangindo ambao ni wenyeji wa wilaya ya Kilwa Lindi,na mmoja wa watoto wake Bi Mariam Amri kushoto, katika kijiji cha kiranjeranje wilayani humo hivi karibuni
WACHUUZI-KITUO CHA MABASI MASASI
,Baadhi ya wachuuzi wadogo wakiwauzia abiria wa basi la Wahida linalofanya safari kati ya Tunduru na D,slaam katika kituo cha mabasi masasi mjini,bidhaa zao,
MAENDELEO YA UJENZI WA MADARAJA
Moja ya kati ya madaraja yaliyojengwa katika barabara kuu ya mangaka masasi ambayo ujenzi wake pamoja na barabara hiyo unalalamikiwa kuwa uko chini ya kiwango, kama yanavyoonekana,
Subscribe to:
Posts (Atom)