Saturday, June 30, 2012

TUKIO LIPO KARIBU............

Ilikuwa tunahesabu mwaka,tukahesabu miezi,hatukuchoka tukahesabu siku,sasa tunasubiri  masaa ambayo si mengi ni machache sana huwezi amini lile tukio kubwa la uzinduzi wa filamu ya adelahida lipo karibu sana.Njoo uwaone wakali Shukran,Jamilah,Pesa Mbili,Big,Bright,Kazimgulu bila kusahau burudani mbali mbali kutoka kundi zima la dreams arts group.Njoo uone show za dansi,show za vichekesho,show za muziki .show za ngoma za utamaduni kutoka kwa mwanawane,show za Michael Jackson,show za sarakasi zilizoenda shule.Haya yote ni Jumapili tarehe 1 Julai,2012 kuanzia saa nane mchana kwenye ukumbi wa Songea Club.Bila kusahau mgeni rasmi atakuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea,Mheshimiwa Mariam M.Dizumba.

Monday, June 25, 2012

TUNAWEZA..........

Hii ilikuwa Uwanja wa Majimaji-Songea kwenye Tamasha Kubwa la Sanaa ambalo lilihusisha wasanii wa muziki,filamu,maigizo,vichekesho na vingine vingi.Lengo likiwa kutoa burudani na sanaa kama ajira na njia ya kuvuna kipato.Matarajio ni kufanya matamasha kama haya mara kwa mara na kuendelea kuwashawishi wadhamini wataweza kutangaza bidhaa zao vizuri.Hawa ni Dreams Arts Group hapa wanacheza muziki katika kunogesha Burudani kwa wakazi wa Ruvuma na maeneo ya jirani.

Monday, June 11, 2012

BIG MAN RECORDS to ONE MORE RECORDS...Guess What Next???? tunakumbushana

Nyimbo hii ili-recodiwa katika studio za One More Records zamani Big Man Records chini ya uongozi wa LOVES BIG mwaka 2009 ikiwa na Msanii Mery Lucos(BSS TOP 5) Soka Star, Bongo Movie star Dannis David.. producer Dimo Debwe. studio zilikuwa maeneo ya posta mpya katika jengo la nedco jijini Dar es salaam.. Tayari maandalizi ya ujio mpya yameelekea kufikia mlangoni.. je, ninikinafuata? tega sikio..!!

Friday, June 8, 2012

KUITAMBULISHA ADELAHIDA

Filamu kuhusu maisha wakati wa utawala wa machifu mwanzoni mwa karne ya 20. Tuna mila na desturi ambazo ni nzuri na zinapaswa kufuatwa na kurithiwa kutoka kizazi kimoja na  kwenda   kingine.Machifu waliaminika kama ni watawala kwa ajili ya kuongoza jamii,kuhakikisha amani na haki.Kuna wakati ilifikia wanatumia madaraka vibaya na kuwa wakatili na kufikia kuwauwa    watu    wasioukuwa na hatia na kuwatenganisha na familia na kuleta mvurugano kwenye yote.Kaa tayari kwa simulizi…

UJIO WA FILAMU YA ADELAHIDA

Kaa tayari kwa Filamu ya Adelahida iliyotayarishwa na Mtayarishaji anayechipukia Shukurani K.Faraji.Ndugu watatu Ade,Lah na Ida wanakuja kukutana tena baada ya kupoteana kwa muda wa miaka ishirini.Kujua kilichosababisha utakiona na ndani ya Filamu hii.Ni filamu iliyotengenezwa kwenye mazingira ya asili katikakati ya misitu maeneo ya Matogoro-Songea.

Thursday, June 7, 2012

ADE NA RAH

Waashiriki wakuu kwenye Filamu ya Adelahida ,Jamila Abdulkarim(ADE) akiwa na Shukurani K.Faraji(RAH) wakisikiliza maelekezo