Tuesday, October 25, 2011

Muuza nyama kutoka moja ya mabucha yaliyopo  Soko Kuu la Manispaa ya Songea aliyefahamika kwa jina moja la Heddy akiuchapa usingizi baada ya kusubiri wateja kwa muda mrefu bila ya mafanikio,ulazi wa kitoweo hicho katika mji wa songea unazidi kupungua kufuatia ongezeko la bei kutoka ths 4000 hadi 5000 kwa kilo.

PAMBANO LA KIRAFIKI

Bondia Mussa Omari wa Songea kushoto,akimpiga ngumi bondia Mohamed Matumla kulia ambaye ni mtoto wa bondia mkongwe Rashid Matumla katika pambano lao lisilokuwa na ubingwa wowote lililofanyika katika uwanja wa majimaji  siku Idd el Fitri mjini Songea juzi,ambapo mabondia hao walitoshana nguvu kwa kutoka sare,
PICHA NO 067,Gari no T554 AVZ linalofanya safari kati ya Msamala na Soko Kuu mjini Songea likiwa limeacha njia na kutumbukia katika mtaro pembezoni mwa barabara kuu ya Songea-Njombe- Makambako katika eneo la Bombambili mjini hapa,ambapo watu 5 walijeruhiwa,

ICE CREAM

,Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Majengo katika Manispaa ya Songea wakila askrim kwa ajili ya kupoza kiu.

Thursday, October 20, 2011

Kijana aliyetuhumiwa kuiba simu ya mama mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja,akipanda gari la polisi baada ya kumuokoa kutokana na kipigo alichokuwa akipata kutoka kwa wananchi wenye hasira kali mijini Songea jana
Kijana aliyeshukiwa kuwa ni kibaka akiwa amelala chini kwa lengo
la kuomba msaada baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa 
wananchi wenye hasira baada ya kijana huyo kutuhumiwa kuiba simu
ya mkononi ya mmoja wa wapita njia karibu na kituo cha daladala 
cha soko kuu la Mjini Songea.
Kijana aliyedhaniwa kuwa ni kibaka akiwa chini kwa ikiwa ni ishara ya kuomba msaada baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi,baada yakutuhumiwa kuiba simuya abiria mmoja  katika kituo cha daladala mjini  songea jana
Msamaria mwema  kulia ambaye hakutaka kutaja jina lake,akimuokoa kijana aliyekuwa akipata kipigo kutoka kwa watu wenye hasira kali,kufuatia kijana huyo kumuibia abiria simu ya mkononi katika kituo cha Daladala  cha soko kuu mjini songea.

Wednesday, October 12, 2011

SIKUKUU YA MASHUJAA-SONGEA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa,akitoa heshima katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa vita ya Majimaji wakati wa siku ya Mashujaa  ambayo kwenye ngazi ya mkoa ilifanyika Mjini Songea.

BAADA YA MLO SHULE INAENDELEA

 wanafunzi wa shule ya msingi kawawa manispaa ya Songea ambao hawakufahamika mara moja ni wa darasa la ngapi wakila kande wakati wa mapumziko yao ya saa nne katika kibanda kimojawapo cha mama lishe kilichopo jirani na shule hiyo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu mjini songea,

MWACHIENI YUPO HURU

,Hakimu mkazi mfawidhi wa mahama ya mkoa Ruvuma,Batisita Muhelela,akiwasihi polisi wasiendelee kumshikilia bw mohamedi nditi aliyekaa chini ambaye alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuvunja na kuiba ambapo aloifutiwa mashitaka baada ya kukosekana ushahidi,

CHINI YA ULINZI


Askari polisi wakimdhibiti Bw Mohamedi nditi katikati ili asikimbie baada ya jaribio lake la kutaka kutoroka chini ya ulinzi wa polisi hao kushindikana jana mbele ya mahakama ya mkoa Ruvuma,

TUKIO LA KIMILA-KILWA

Baadhi ya wajukuu kati ya wajukuu 100 wa marehemu Jumbe Mshamu mmanja,wakishika jiwe mojawapo la kaburi la babu yao aliyefariki miaka 150 iliyopita ambalo liko zaidi ya km 5 kutoka barabara kuu ya Kibiti Lindi eneo la kijiji cha Kiranjeranje wilayani Kilwa juzi ikiwa ni shara ya kumkumbuka na kumuombea kwa lengo la kupata baraka zake,

TUKIO LA KIMILA-KILWA

Mzee Abderehaman Amri,kulia akicheza ngoma ya kindimba linalochezwa na kabila la wangindo ambao ni wenyeji wa wilaya ya Kilwa Lindi,na mmoja wa watoto wake Bi Mariam Amri kushoto, katika kijiji cha kiranjeranje wilayani humo hivi karibuni

WACHUUZI-KITUO CHA MABASI MASASI


,Baadhi ya wachuuzi wadogo wakiwauzia abiria wa basi la Wahida linalofanya safari kati ya Tunduru na D,slaam katika kituo cha mabasi masasi mjini,bidhaa zao,

MAENDELEO YA UJENZI WA MADARAJA

Moja ya kati ya madaraja yaliyojengwa katika barabara kuu ya mangaka masasi ambayo ujenzi wake pamoja na barabara hiyo unalalamikiwa kuwa uko chini ya kiwango, kama yanavyoonekana,