Sunday, March 31, 2013

Mbuga ya Selous,Likuyu Sekamaganga-Namtumbo

Eneo la Hifadhi ya Mbuga ya wanyama ya Selous,Likuyu Sekamaganga-Namtumbo.Utawaona wanyama wa aina mbalimbali kwa ajili ya Utalii wa Ndani na wa Nje.Karibuni tutembelee mbuga zetu kwa mapumziko na maendeleo ya Taifa Letu.

x

MPIGA GUITAR LA SOLO

Mpiga Guitar la Solo aliyebobea kwenye chombo hicho almaarufu Mtumishi Zenda.Namnukuu "Napenda sana wasanii wa muziki wa kizazi kipya wajifunze ala mbalimbali za muziki,sababu itafikia wakati urithi huu wa kupiga ala ukapotea na sehemu kubwa ya wanamuziki wanaopiga ala hizi ni wazee".
Zenda ni hazina kwa upande wa guitar na kwa yeyote ambaye yupo tayari kujifunza misingi ya upigaji wa guitar milango ipo wazi.
Pia kwa mahitaji ya kuingiza guitar kwenye studio za kurekodia muziki anamudu vilivyo
Zenda anapatikana katika Mji wa Songea contacts 0687631828
email:        nicholauszenda@gmail.com

Thursday, March 21, 2013

COMMING SOON.........AFRICAN BIG MAMA

Washiriki wakuu wa Filamu ya African Big Mama,Mzee Jengua na Shukurani Kasim wakiwa kwenye    Location huko Mkongo-Namtumbo.
African Big Mama inamzungumzia mwanamke mwanaharakati ambaye yupo mstari wa mbele kuwatetea wanawake,watoto na wengine.Harakati zake zinapingana na matendo ya uonevu ya mume wake ambaye ni Kiongozi wa Kimila(Chifu).Subiri kuona ni lipi litatokea kwenye filamu hii ya mwanamke shujaa!

Wednesday, March 20, 2013

ELIZA ACCESSORIES SHOP


Inapatikana Stendi Kuu ya Songea Mbele ya Ofisi ya Sumry High Class

Kwa Huduma za M-pesa,Tigo Pesa,Airtel
Simu za aina mbalimbali
Phone Accessories

 Bidhaa zetu ni bora na bei zetu ni nafuu sana.
 Tunafanya kazi siku zote za wiki
 Kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili na nusu za usiku
 Karibu sana 

SINIA


Comming Soon 



Filamu ya vichekesho(comedy) iliyojaa visa kibao inayowahusisha kijana Chidy na binti Sinia.Chidy na Sinia wote ni wanafunzi ambao wanaishi kwa wazazi wao.Familia hizi mbili zinazokaa kwenye jamii moja zina hali ya kipato(uchumi) tofauti.

Monday, March 18, 2013

ASATA




ASATA
Asata ni Mwanafunzi wa Uuguzi(Nursing) amekuja Songea kufanya mafunzo ya Vitendo.Akiwa safarini kuja kuanza mafunzo anakutana na misukosuko na inamlazimu kukaa kwenye pori kwa siku kadhaa.Anapofanikiwa kutoka porini anakutana na misukosuko mingine inapelekea mahusiano yake na mpenzi wake kuwa kwenye mashaka.Fuatilia kisa hiki kwenye Filamu hii ya Asata........