Saturday, June 30, 2012
TUKIO LIPO KARIBU............
Ilikuwa tunahesabu mwaka,tukahesabu miezi,hatukuchoka tukahesabu siku,sasa tunasubiri masaa ambayo si mengi ni machache sana huwezi amini lile tukio kubwa la uzinduzi wa filamu ya adelahida lipo karibu sana.Njoo uwaone wakali Shukran,Jamilah,Pesa Mbili,Big,Bright,Kazimgulu bila kusahau burudani mbali mbali kutoka kundi zima la dreams arts group.Njoo uone show za dansi,show za vichekesho,show za muziki .show za ngoma za utamaduni kutoka kwa mwanawane,show za Michael Jackson,show za sarakasi zilizoenda shule.Haya yote ni Jumapili tarehe 1 Julai,2012 kuanzia saa nane mchana kwenye ukumbi wa Songea Club.Bila kusahau mgeni rasmi atakuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea,Mheshimiwa Mariam M.Dizumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment