Saturday, June 30, 2012
TUKIO LIPO KARIBU............
Ilikuwa tunahesabu mwaka,tukahesabu miezi,hatukuchoka tukahesabu siku,sasa tunasubiri masaa ambayo si mengi ni machache sana huwezi amini lile tukio kubwa la uzinduzi wa filamu ya adelahida lipo karibu sana.Njoo uwaone wakali Shukran,Jamilah,Pesa Mbili,Big,Bright,Kazimgulu bila kusahau burudani mbali mbali kutoka kundi zima la dreams arts group.Njoo uone show za dansi,show za vichekesho,show za muziki .show za ngoma za utamaduni kutoka kwa mwanawane,show za Michael Jackson,show za sarakasi zilizoenda shule.Haya yote ni Jumapili tarehe 1 Julai,2012 kuanzia saa nane mchana kwenye ukumbi wa Songea Club.Bila kusahau mgeni rasmi atakuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea,Mheshimiwa Mariam M.Dizumba.
Wednesday, June 27, 2012
Monday, June 25, 2012
TUNAWEZA..........
Hii ilikuwa Uwanja wa Majimaji-Songea kwenye Tamasha Kubwa la Sanaa ambalo lilihusisha wasanii wa muziki,filamu,maigizo,vichekesho na vingine vingi.Lengo likiwa kutoa burudani na sanaa kama ajira na njia ya kuvuna kipato.Matarajio ni kufanya matamasha kama haya mara kwa mara na kuendelea kuwashawishi wadhamini wataweza kutangaza bidhaa zao vizuri.Hawa ni Dreams Arts Group hapa wanacheza muziki katika kunogesha Burudani kwa wakazi wa Ruvuma na maeneo ya jirani.
Monday, June 11, 2012
BIG MAN RECORDS to ONE MORE RECORDS...Guess What Next???? tunakumbushana
Nyimbo hii ili-recodiwa katika studio za One More Records zamani Big Man Records chini ya uongozi wa LOVES BIG mwaka 2009 ikiwa na Msanii Mery Lucos(BSS TOP 5) Soka Star, Bongo Movie star Dannis David.. producer Dimo Debwe. studio zilikuwa maeneo ya posta mpya katika jengo la nedco jijini Dar es salaam.. Tayari maandalizi ya ujio mpya yameelekea kufikia mlangoni.. je, ninikinafuata? tega sikio..!!
Friday, June 8, 2012
KUITAMBULISHA ADELAHIDA
Filamu kuhusu maisha wakati wa utawala wa
machifu mwanzoni mwa karne ya 20.
Tuna
mila na desturi ambazo ni nzuri na zinapaswa kufuatwa na kurithiwa kutoka
kizazi kimoja na kwenda kingine.Machifu waliaminika kama ni watawala kwa ajili
ya kuongoza jamii,kuhakikisha amani na haki.Kuna wakati ilifikia wanatumia
madaraka vibaya na kuwa wakatili na kufikia kuwauwa watu wasioukuwa na hatia na
kuwatenganisha na familia na kuleta mvurugano kwenye yote.Kaa tayari kwa
simulizi…
UJIO WA FILAMU YA ADELAHIDA
Kaa tayari kwa Filamu ya Adelahida iliyotayarishwa na Mtayarishaji
anayechipukia Shukurani K.Faraji.Ndugu watatu Ade,Lah na Ida wanakuja
kukutana tena baada ya kupoteana kwa muda wa miaka ishirini.Kujua
kilichosababisha utakiona na ndani ya Filamu hii.Ni filamu
iliyotengenezwa kwenye mazingira ya asili katikakati ya misitu maeneo ya
Matogoro-Songea.
Thursday, June 7, 2012
ADE NA RAH
Waashiriki wakuu kwenye Filamu ya Adelahida ,Jamila Abdulkarim(ADE) akiwa na Shukurani K.Faraji(RAH) wakisikiliza maelekezo
Subscribe to:
Posts (Atom)