Muendesha pikipiki akionesha manjonjo yake ya kuchezea pikipiki kwenye viwanja vya Zimanimoto-Songea.Hii ilikuwa ni kwenye Tamasha la Burudani na Michezo ambalo lilifanyika Jumapili tarehe 28 Aprili,2013.Tamasha hili liliwahusisha wasanii wa filamu na muziki wa ndani na nje ya Songea ambapo kwa wakati tofauti walitoa burudani ambayo iliwafurahisha wakazi wa ndani na nje ya Songea.Tutaendelea kuliona hili Tamasha kila wiki ya mwisho wa mwezi na tunategemea litazidi kuboreshwa chini ya usimamizi wa Equator Night Club ,Radio Jogoo FM na Michango kutoka kwa wadau wote wa michezo,sanaa na burudani.
No comments:
Post a Comment