Monday, April 29, 2013

Bonanza la Burudani na Michezo

Muendesha pikipiki akionesha manjonjo yake ya kuchezea pikipiki kwenye viwanja vya Zimanimoto-Songea.Hii ilikuwa ni kwenye Tamasha la Burudani na Michezo ambalo lilifanyika Jumapili tarehe 28 Aprili,2013.Tamasha hili liliwahusisha wasanii wa filamu na muziki wa ndani na nje ya Songea ambapo kwa wakati tofauti walitoa burudani ambayo iliwafurahisha wakazi wa ndani na nje ya Songea.Tutaendelea kuliona hili Tamasha kila wiki ya mwisho wa mwezi na tunategemea litazidi kuboreshwa chini ya usimamizi wa Equator Night Club ,Radio Jogoo FM na Michango kutoka kwa wadau wote wa michezo,sanaa na burudani.

Friday, April 26, 2013

Pata ramani yako

Mfano wa nyumba kazi iliyofanywa na Royal framing and photo solution chini ya Mkurugenzi Yusuph Kondela Mange. contacts +255782350152

Tupendezeshe Mji wetu

Mfano wa nyumba kazi iliyofanywa na Royal framing and photo solution chini ya Mkurugenzi Yusuph Kondela Mange. contacts +255782350152

Usanifu na Ubunifu wa Majengo

Mfano wa nyumba kazi iliyofanywa na Royal framing and photo solution chini ya Mkurugenzi Yusuph Kondela Mange. contacts +255782350152

Wednesday, April 24, 2013

Majengo Mitumbani

Mtaa wa Kotaz Majengo eneo ambalo ni maarufu kama Majengo mitumbani.Hapa unaweza kujipatia bidhaa mbalimbali za mitumba kama nguo,viatu na mikoba n.k.
Kwa siku ya Jumapili barabara hii hufungwa na kunakuwa na mnada wa bidhaa za chakula kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kama,mboga ,nafaka,matunda na viungo.

Monday, April 22, 2013

Muonekano Tofauti..........

 Salmada(Kihongolo Binti Msukule) kwenye uchukuaji wa picha za filamu ya Kihongolo Binti Msukule  huko Mateka,Kisiwani-Songea.

Friday, April 19, 2013

Kazi na Majadiliano....

Mwenyasa Nyasa Boy mtayarishaji wa filamu ya (Kihorongo Binti Msukule) akiwa na Salmada wakijadiliana kwenye tukio katika kuhakikisha tunapata kitu bora

Salmada anakimbiza

Salmada(Kihorongo),Msanii wa filamu ambaye anafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu na ameshiriki kwenye filamu kadhaa.Yeye ni mmoja wa washiriki wakuu wa filamu ya Kihorongo Binti Msukule.

KIHORONGO BINTI MSUKULE


Salmada (upande wa kulia) akiwa kwenye tukio la uchukuaji picha za filamu inayoenda kwa jina la Binti Kihongoro Binti Msukule.

Tuesday, April 9, 2013

DANGEROUS CAMP

Filamu ya Dangerous Camp imeanza kusambazwa rasmi na unaweza kuipata  madukani ,pata nakala yako na uburudike,ufurahie na ujifunze kwenye filamu iliyosheheni matukio ya mapigano na mengine mengi ya kuvutia.
Usikose!!!!

Sunday, March 31, 2013

Mbuga ya Selous,Likuyu Sekamaganga-Namtumbo

Eneo la Hifadhi ya Mbuga ya wanyama ya Selous,Likuyu Sekamaganga-Namtumbo.Utawaona wanyama wa aina mbalimbali kwa ajili ya Utalii wa Ndani na wa Nje.Karibuni tutembelee mbuga zetu kwa mapumziko na maendeleo ya Taifa Letu.

x

MPIGA GUITAR LA SOLO

Mpiga Guitar la Solo aliyebobea kwenye chombo hicho almaarufu Mtumishi Zenda.Namnukuu "Napenda sana wasanii wa muziki wa kizazi kipya wajifunze ala mbalimbali za muziki,sababu itafikia wakati urithi huu wa kupiga ala ukapotea na sehemu kubwa ya wanamuziki wanaopiga ala hizi ni wazee".
Zenda ni hazina kwa upande wa guitar na kwa yeyote ambaye yupo tayari kujifunza misingi ya upigaji wa guitar milango ipo wazi.
Pia kwa mahitaji ya kuingiza guitar kwenye studio za kurekodia muziki anamudu vilivyo
Zenda anapatikana katika Mji wa Songea contacts 0687631828
email:        nicholauszenda@gmail.com

Thursday, March 21, 2013

COMMING SOON.........AFRICAN BIG MAMA

Washiriki wakuu wa Filamu ya African Big Mama,Mzee Jengua na Shukurani Kasim wakiwa kwenye    Location huko Mkongo-Namtumbo.
African Big Mama inamzungumzia mwanamke mwanaharakati ambaye yupo mstari wa mbele kuwatetea wanawake,watoto na wengine.Harakati zake zinapingana na matendo ya uonevu ya mume wake ambaye ni Kiongozi wa Kimila(Chifu).Subiri kuona ni lipi litatokea kwenye filamu hii ya mwanamke shujaa!

Wednesday, March 20, 2013

ELIZA ACCESSORIES SHOP


Inapatikana Stendi Kuu ya Songea Mbele ya Ofisi ya Sumry High Class

Kwa Huduma za M-pesa,Tigo Pesa,Airtel
Simu za aina mbalimbali
Phone Accessories

 Bidhaa zetu ni bora na bei zetu ni nafuu sana.
 Tunafanya kazi siku zote za wiki
 Kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili na nusu za usiku
 Karibu sana 

SINIA


Comming Soon 



Filamu ya vichekesho(comedy) iliyojaa visa kibao inayowahusisha kijana Chidy na binti Sinia.Chidy na Sinia wote ni wanafunzi ambao wanaishi kwa wazazi wao.Familia hizi mbili zinazokaa kwenye jamii moja zina hali ya kipato(uchumi) tofauti.

Monday, March 18, 2013

ASATA




ASATA
Asata ni Mwanafunzi wa Uuguzi(Nursing) amekuja Songea kufanya mafunzo ya Vitendo.Akiwa safarini kuja kuanza mafunzo anakutana na misukosuko na inamlazimu kukaa kwenye pori kwa siku kadhaa.Anapofanikiwa kutoka porini anakutana na misukosuko mingine inapelekea mahusiano yake na mpenzi wake kuwa kwenye mashaka.Fuatilia kisa hiki kwenye Filamu hii ya Asata........